Kiongozi
wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe jana tarehe 7/6/2016 aliitwa
Polisi na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam ACP
Camilius Wambura.
Kwa
mujibu wa Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho Ado
Shaibu, amesema ACP Wambura amemuita Zitto Kabwe kuhojiwa ikiwa ni siku
moja imepita tangu azindue operesheni Linda Demokrasia ambayo
inatarajiwa kuzunguka nchi nzima kupinga ukandamizwaji wa Demokrasia
nchini
Amesema
licha ya Zitto kuitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es
salaam Wambura aliomba Zitto asiende jana kwa kuwa ni karibu na masaa
ya kufuturu na kumtaka aende leo saa tatu asubuhi.
Kwa
upande mwingine Shaibu amesema Chama cha ACT-Wazalendo kitawasiliana
na wanasheria wao ili kupata tafsiri ya kimahakama ya uhalali wa jeshi
la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inatambuliwa na
kulindwa na katiba.