Taarifa hiyo ya Bunge imekuja siku moja baada ya taarifa
kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kuwa kiongozi huyo yuko
katika hali mbaya, jambo ambalo limeelezwa siyo kweli. Takribani wiki ya
tatu sasa, Ndugai hajaonekana bungeni.
Mkuu wa Kitengo cha
Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge, Owen Mwandumbya alisema jana kuwa
kiongozi huyo amekwenda India kwa uchunguzi.
Alisema Spika aliporejea kutoka India Desemba mwaka jana, alitakiwa kurudi tena baada ya muda kwa ajili ya uchunguzi.
“Atarudi muda wowote kuanzia hivi sasa kwani yuko nchini India,” alisema Mwandumbya.
Alifafanua kuwa hali ya spika iko vizuri na hivi sasa anafanya mambo ya kawaida ili aweze kurejea nchini.
Mwaka
jana baada ya Ndugai kuwasili kutoa India, alisema afya yake iko imara
na anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na madaktari.