Watuhumiwa wa mauaji Makete waachiwa kwa dhamana, Wananchi watangaza kuwaua (Audio)

Kufuatia Mauaji yaliyotokea mwanzoni mwa mwezi huu katika kijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilayani Makete ambapo Mtoto mwenye miaka 17 aliuwawa kwa kupigwa na Miwa pamoja na Miti kwa tuhuma za wizi, hatimaye watuhumiwa wa mauaji hayo Familia ya Bw. Goden Sanga wamepewa dhamana na Mahakama jambo ambalo limezua masikitiko kwa wananchi na kuagiza kutoiona familia ya Mtuhumiwa wa Mauaji hayo kijijini hapo

Wananchi waliojawa na Hasira jana waliitisha mkutano Mkuu wa kijiji uliomshirikisha Mh.Diwani wa kata hiyo Augustino Tweve ambaye alitolea ufafanuzi wa watuhumiwa hao kupewa dhamana ilihali wanadaiwa kumuua marehemu

Huku Wananchi hao wakiwa na Hasira kwa muda mrefu katika mkutano ulioanza majira ya saa 05:09 asubuhi hadi saa 11 jioni huku wengine wakitokwa na machozi, walisema jeshi la polisi likifika kijijini hapo linatakiwa kuwachukua watuhumiwa na kuwarudisha tena Rumande na hawataki kuwaona kijijini hapo kwa wakati huu ambao bado wanamajonzi ya Kijana wao aliyeuwawa kwa kupigwa, huku inaelezwa kuwa Watuhumiwa hao kwa sasa wanatuhumiwa kwa kesi ya Mauaji ya kutokusudia jamabo ambalo linapingwa vikali na wananchi hao
Wananchi hao wamesema kuwa Bw. Golden amekuwa na kawaida ya kuwapiga na kuwaumiza watu mbalimbali tokea kipindi cha nyuma hivyo ni kawaida yake kufanya masuala ya unyanyasaji kama hayo kijijini hapo

Mwenyekiti wa kijiji cha Utweve pamoja  na Mh.Diwani wa kata ya Ukwama walitishia kujiuzulu mbele ya wananchi endapo hakutachukuliwa maamuzi ya watuhumiwa wa Mauaji hayo kukamatwa na kurudishwa Rumande

Diwani wa kata ya Ukwama Mh.Agustono Tweve aliliomba jeshi la Polisi kufuata maamuzi ya wananchi kuhakikisha wanawatafuta watuhumiwa wa Mauaji hayo na kuondoka nao kuwapeleka rumande ili wasionekane machoni pa wananchi na upelelezi uchukuliwe upya kwani wanawatuhumu watuhumiwa kwamba wameua kwa kukusudia na sio kwa kutokusudia

Hata hivyo Jeshi la polisi kitengo cha Upelelezi lililazimika kuwasikiliza wananchi hao kwa kile wanachokitaka kwani usalama wa Watuhumiwa haupo endapo watasalia kijijini hapo badala yake warudi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama

Sikiliza sauti hapa chini
Shukrani kwa Kitulo Fm


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo