Wananchi hao wamekumbwa na majanga hayo katika kijiji cha Kros ambako wamepewa hifadhi na wenyeji.
Imedaiwa kuwa majira ya saa nane za usiku wa juzi nyumba
waliyokuwa wamelala iligongwa milango na kwamba walipokaidi kufungua,
wavamizi hao waliupiga kwa nguvu kwa lengo la kutaka kuivunja.
Mashuhuda walisimulia kuwa hali hiyo ilisababisha taharuki.
Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) walifika kuokoa jahazi
baada ya kupigiwa simu na mmoja wa wakazi wa kijiji, hicho kwa lengo la
kuomba msaada wakihofia kuchinjwa, imeelezwa.
Mmoja wa wananchi hao waliokimbia kuchinjwa, Mponile Mluafu
aliliambia Nipashe jana kijijini hapo kuwa usiku wa kumkia juzi,
kulitokea tafrani baada ya watu wasiofahamika kugonga nyumba
walimohifadhiwa wageni hao na kulazimisha wafunguliwe.
Mluafu alisema tukio hilo lilizusha hofu kwa kuwa watuhao
baada ya kugonga na kutofunguliwa mlango, walitumia nguvu kutaka
kuuvunja lakini majirani waliosikia kishindo hicho walipiga simu kambi
ya Jeshi iliyopo karibu na muda mfupi kikosi cha askari wa Jeshi
kilifika.
“Hawa watu nadhani walisikia taarifa ya simu wakatokomea
kusikojulikana, na hata wanajeshi walipofika hawakukuta mtu eneo hilo,”
alisema Mluafu.
Mluafu alisema hali imekuwa tete kwa wageni hao kwa kuwa
baada ya tukio hilo, wenyeji walikimbia nyumba hiyo na kuwaacha peke yao
kwa kuhofia kuchinjwa.
Mluafu alisema hali imekuwa tete kwa wageni hao kwa kuwa
baada ya tukio hilo, wenyeji walikimbia nyumba hiyo na kuwaacha peke yao
kwa kuhofia kuchinjwa.
Akizungumzia katika makazi mapya, Maimuna Said alisema hali
ni ngumu kwani wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo chakula,
malazi na kwamba hata maisha yao kwa ujumla bado yapo hatarini.
Kunyeta Hossen aliiomba serikali kuwapa msaada wa vyakula na malazi ili waepukane na maradhi kama kipindupindu.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee,
Ummy Mwaimu akiambatana na Mbunge wa Muheza, Adadi Rajab, Mbunge wa
Handeni, Omari Kigoda na Mbunge wa Pangani, Jumaa Aweso walitembelea
makazi ya waathirika hao wa mauaji jana ili kujionea hali halisi.