WALIMU wanne wa sekondari Jumapili walijipata katika seli za
polisi mjini Murang’a Kenya baada ya kupigana kwa kudaiwa kutofautiana kuhusu
mlo wa kuku katika baa moja ya mji huo.
Walimu hao ambao walikuwa wakiburudika pamoja kwa
vilewesho walikamatwa kwa madai ya kuvuruga amani ya umma waliporushiana
makonde na kusababisha uharibifu wa mali katika baa hiyo.
Kwa mujibu wa afisa mpelelezi katika kisa hicho Bw
Judah Muriuki, walimu hao wa kiume walitofautiana kuhusu mlo wa kuku;
jogoo mmoja wa kilo nne.
“Shida ilitokea wakati mchuuzi wa kuku aliingia
akitafuta wateja wa jogoo kadhaa aliokuwa nao. Alipofika katika meza
ambayo waalimu hao
walikuwa, kukatokea kejeli za ni nani angeweza kumaliza kuku huyo akiwa peke yake,” akasema.
walikuwa, kukatokea kejeli za ni nani angeweza kumaliza kuku huyo akiwa peke yake,” akasema.
Mwalimu mmoja anasemekana kuwa alidai angeweza
kumaliza jogoo huyo akiwa peke yake, bora tu iwe amekaangwa vizuri na
atiwe supu vikombe viwili.
Kulingana na Bw Muriuki, wenzake mwalimu huyo walisema hakuna namna hilo lingewezekana.
“Ndipo mwalimu huyo aliwaagiza wenzake wanunue jogoo
huyo aliyekuwa akiuzwa kwa Sh1,200 na ikiwa hataweza kummaliza kama
alivyokuwa akidai, basi yeye mwenyewe angetoa Sh5,000 kama fidia kwao,”
akasema afisa huyo wa polisi.
Inasemekana kuwa kuku huyo alichinjwa na akakatwa vipande kadhaa na akatayarishwa namna mwalimu huyo alikuwa ameagiza.
“Kutayarishwa, nyama ililetwa katika meza hiyo.
Mwalimu aliyekuwa amedai angeimaliza akaanzana nayo. Akaanza na vipande
vya miguu,
akaenda kwa kipapatio na kisha akachukua kipande kimoja cha mgongo,” akaarifu afisa huyo wa polisi.
akaenda kwa kipapatio na kisha akachukua kipande kimoja cha mgongo,” akaarifu afisa huyo wa polisi.
Ni wakati walimu wenzake waliona kana kwamba mwenzao
angeimaliza nyama hiyo ya kuku huyo ambapo waliirukia nyama hiyo na
wakaanza kuibishania na hatimaye vita vya makonde na urushaji chupa
ukatokea.
Hasara
Kwa mujibu wa Bw Muriuki, walimu wenzake walionelea
wangeenda hasara ikiwa mwenzao angeikula nyama hiyo animalize peke yao
ilihali wao ndio walikuwa wameinunua.
“Lakini ajabu ni kuwa baada ya kuwakamata, mwalimu
huyo alidokeza kuwa hakuna uwezekano angeimaliza nyama hiyo na alikuwa
anawaza jinsi ya kupata fedha za kuwalipa wenzake kwani alikuwa
amelemewa katika kilo moja tu na kiasi kidogo juu yake,” akasema.
Hata hivyo, walimu hao waliachiliwa Jumatatu asubuhi
bila ya mashtaka yoyote baada ya muungano wa walimu (KUPPET) tawi la
Murang’a kuingilia kati.
Hata hivyo, duru za kuaminika ziliashiria kuwa walimu
hao walitoa kitu kidogo cha kununua msamaha ndipo wakaachiliwa, jambo
ambalo wote walikana.
“Hakuna pesa zozote zilitolewa na upande wowote. Tuliamua tu kuwasamehea ikizingatiwa kuwa walikuwa shereheni kama wanataaluma
lakini tofauti kidogo zikazuka,” akasema Bw Muriuki.
lakini tofauti kidogo zikazuka,” akasema Bw Muriuki.
