Siku hizi MUNGU haogopwi, Wezi waiba kituo cha Udiakonia Tandala, Sikiliza hapa ilikuwaje?

Wananchi Wa kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kufanikiwa kudhibiti mtandao wa wizi uliopo katika kata hiyo.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa kituo cha Udiakonia Tandala Mch. Sedekia Luvanda alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu juu ya tukio la wizi lililotokea usiku wa kuamkia jumatatu ya wiki hii katika kituo hicho ambapo watu wasiojulikana walibomoa baadhi ya majengo katika kituo hicho na kufanikiwa kuondoka na baadhi ya vitu ikiwemo kompyuta mpakato na fedha na baadhi ya nyaraka muhimu zilizokuwa zimehifadhiwa katika ofisi zilizovunjwa.

Pamoja na kutoa wito huo Mchg.Luvanda ameelezea jinsi tukio hilo lilivyotokea na maeneo yaliyoathirika zaidi kwa kusema zimevunjwa ofisi na wezi hao kuiba fedha na laptop.

Amebainisha kuwa ni vigumu kuzungumzia moja kwa moja hasara iliyopatikana kutokana na wizi huo kwani kituo hicho bado kinaendelea na uchunguzi juu ya hasara iliyojitokeza kufuatia tukio hilo.

Mchg Luvanda amesema kuendelea kujitokeza kwa matukio ya wizi katika kata ya Tandala ni ishara kuwa kuna watu wenyeji wanaoshirikiana na wahalifu hao kwani mtandao wa wizi umeonekana kukua kila kukicha.

Hapa chini kuna sauti za tukio hilo zisikilize

Na Fadhili Lunati


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo