Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wafuasi wa CHADEMA

Polisi mkoani Kahama wametumia mabomu ya machozi kutawanya makundi ya wananchi wanaokutwa wamekusanyika katika maeneo mbalimbali.

Mabomu hayo yameendelea kurindima katika viwanja vya CDT ili kuwatawanya wananchi hao waliokusanyika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa Chadema.

Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo kuanzia saa 9.00 alasiri kabla ya polisi kuupiga marufuku na jeshi hilo kuzuia mikutano mingine kama hiyo nchini.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni la leo na Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya amepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadharahadi hali ya usalama itakapotengemaa.

Amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yoyote au chama chochote kitakachokaidi agizo hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo