Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) mkoani Mtwara limelazimika
kusimamisha Magari na Pikipiki kuwashusha watu ili wajumuike katika
kufanya usafi unaofanyika kila mwisho wa mwezi baada ya zoezi hilo
kuonekana kusuasua na kufanywa na wananchi wachache zikiwemo taasisi za
serikali.
Akiongoza zoezi hilo la kufanya usafi Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima
Dendego amesifu taasisi zilizojitokeza yakiwemo majeshi ambayo
yamesaidia watu wengi kujitokeza na kufanya usafi.
Wakizungumzia usafi huo wa mazingira baadhi ya wananchi wamesifu
zoezi hilo na kutaka wananchi kujitokeza kila mwisho wa mwezi wingi ili
kufanya usafi ambao ni muhimu kwa afya.
Zoezi la kufanya usafi katika mkoa wa mtwara limekuwa
likihamasishwa sana na vyombo vya habari vilivyopo mkoani humo,na
ikumbukwe, lilizinduliwa na Mh Rais John Pombe Magufuli Disemba tisa
mwaka jana.