Kufuatia kuzimia kwa baadhi wanafunzi katika shule ya msingi Tandala iliyopo kijiji cha Tandala kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe kumepelekea wanafunzi waliokumbwa na tatizo hilo kushindwa kufanya mitihani ya kumaliza mhula wa kwanza.
Hayo yamethibitishwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwl. Yohanes Chaula alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu aliyefika shuleni hapo kutaka kujua ukweli wa taarifa zilizozagaa mitaani kuwa wanafunzi wanazimia ovyo shuleni hapo kama zina ukweli.
Mwalimu mkuu huyo amekiri kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaozimia na kwa sasa imefikia wanafunzi 11 na tayari wanafunzi sita wapo hospitalini kwa matibabu, wanne wapo nyumbani na mwanafunzi mmoja yupo shuleni.

Aidha mwalimu Chaula amesema amekutana na wazazi wa watoto wanaozimia shuleni hapo na kwa pamoja kuazimia waendelee kupatiwa matibabu
Sauti iko hapa chini:-
Na Asukile Mwalwembe