Diwani afumaniwa akimbaka binti wa miaka 14

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Diwani wa kata ya Mtibwa wilayani Mvomero (Chadema), Lucas Edward (38) maarufu kwa jina la Mwakambaya kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 14 mkazi wa Turiani wakiwa katika nyumba ya kulala wageni.

Kamanda Ulrich Matei alisema jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba katika nyumba hiyo ya kulala wageni kuna mtu ameonekana akiwa na binti mdogo ndipo askari walipofuatilia nyendo zake na kumkamata.

Alisema askari baada ya kufika katika nyumba hiyo ya kulala wageni ya Baraka walimkuta mtuhumiwa huyo akiwa na binti huyo chumbani na kwamba uchunguzi wa kitabibu unaendelea ili kubaini uhalisia.

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Mvomero, Mrisho Ramadhani alikiri kukamatwa kwa diwani huyo na kwamba mpaka sasa hajafahamu kosa alilokamatiwa.

Chanzo: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo