Akiongea na East Afrika Television Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji mkoa wa Ilala, Mboje Kanga, amesema tukio hilo lilitokea jana usiku, na mpaka sasa hawajapata idadi kamili ya watu waliokuwa kwenye boti hiyo, wala mmiliki wake bado hajajulikana.
“Mpaka sasa hatuna taarifa rasmi
ila tukio lilitokea usiku, ila ni kwamba kulikuwa na boti inavusha watu
feri, na idadi kamili ya waliokuwa kwenye boti hilo haijapatikana, na
hata kilichotokea rasmi bado hatujajua, ila kuna maiti mbili
zimepatikana mmoja anaitwa Shangali Ibrahim Bimbwa, na mwengine anaitwa
Thomas Beatus Nyoni, na kuna watu watatu inasemekana wameokolewa ila
hatujawapata, inaonekana walikimbia baada ya tukio”, alisema Kamanda Mboje.
Kamanda Mboje amesema huenda watu hao walikimbia baada ya kugundua ni kosa kuvusha watu kwa boti katika eneo hilo, na mpaka sasa shughuli za uchunguzi zinaendelea sambamba na kutafuta miili ya watu wengine,
Mtumbwi huo unasadikika kubeba watu
zaidi ya 16 ambao baadhi yao wametoka wazima.
Siku
ya jana Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifanikiwa kuwapata watu nane
ambapo mmoja wao alipoteza maisha. kutokana na changamoto ya giza
shughuli ya uokoaji iliahirishwa na ikaendelea leo May 28 2016 ambapo
miili mingine ilipatikana na kufikia jumla ya miiili ya watu watano.