Mbunge
wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe
ametumia ukurasa wake wa facebook kuandika mtazamo wake baada ya Rais
Magufuli kufanya maamuzi hayo .
“Uamuzi
wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja –
hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata
aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale
vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha
Uongozi ‘ no nonsense “
