MAKAMU
Mkuu wa Shule ya Sekondari Usevya katika Halmashauri ya Mpimbwe
wilayani Mlele , Makonda Ng’oka “Membele” (34) amefikishwa katika
Mahakama ya mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake.
Mshtakiwa
huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo,
Chiganga Tengwa ambapo alikana shitaka lake na yupo nje baada ya
kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kulipa kiasi cha Sh 3,000,000
mahakamani.
Mwendesha
Mashtaka, Wakili wa Serikali, Gregory Mhangwa alidai mahakamani hapo
kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika shule ya sekondari Usevya kati
ya Novemba 2015 na Aprili 2016.
Alieleza
mahakamani hapo kwamba katika kipindi hicho mshtakiwa alimuingilia
mwanafunzi wake huyo kinyume cha maumbile. Hakimu Tengwa aliahirisha
shauri hilo hadi Juni 26 , mwaka huu litakapotajwa tena.
Inadaiwa
kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule
hiyo kunafuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano katika
shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya
kuwalawiti wanafunzi wake.
Kufuatia
msimamo wa wanafunzi hao iliwalazimu Ofisa Elimu mkoa wa Katavi,
Everest Hunji na Mkurugenzi Mtendaji Halmashari ya Mpimbwe wilayani
Mlele, Evaristo Kiwale kufika shuleni hapo Jumatatu jioni na kuzungumza
na wanafunzi hao.
Wanafunzi
hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni
adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, Kiwale
alisema vitendo vya ushoga havikubaliki na kwamba tayari hatua stahiki
zimeshachukuliwa za kumpeleka katika vyombo vya kisheria.
“Msitaharuki mnapomuona mwalimu huyo mitaani msidhani hajachukuliwa hatua yoyote ile,” alisisitiza.