Mkuu wa wilaya afunga shule nane Kyela

MAWASILIANO katika barabara kuu ya kutoka Kyela Mjini kuelekea Mji wa Ipinda hadi Matema yamekatika ,kutokana na mafuriko ambayo yamesababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Mbeya ,wakati huo shule  nane za msingi na sekondari zikifungwa baada ya kujaa maji na nyingine wanafunzi kukosa mahali pa kupita kutokana na mafuriko hayo.

Dk Thea Ntala ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Wilaya ya Kyela  na ndiye Mkuu wa Wilaya ya hiyo, anasema ametoa amri ya kufunga shule tano za msingi na tatu za sekondari ambazo ni Mwaya , Bujonde na Kajunjumele baada ya baadhi ya shule hizo kujaa maji na nyingine wanafunzi kushindwa kupita baada ya madaraja ya mito wanayovuka kujaa  maji,  Pia anaiomba serikali kuisaidia Halmashauri hiyo tani tano za chakula kwaajili ya tahadhari lakini akadai kuwa kwa sasa Wilaya hiyo haina njaa.

Pamoja na haya Mkuu huyu wa Wilaya amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Clemence Kasongo, kumchukulia hatua  Mkuu wa Shule ya Sekondari  Mwaya kutoka na uzembe wa kusababisha vitendea kazi vya shule hiyo zikiwemo Komputa na vitabu kulowana bila kuchukua tahadhari huku akijua kuwa shule hiyo kila mwaka inakumbwa na mafuriko.

Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Kyela wanaiomba serikali kuinua barabara ya kutoka Kyela mjini kuelekea  miji ya Ipinda na Matema ili kuepusha adha ya kukatika kwa mawasiliano.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo