Hii hapa kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Iringa

15/04/2016 Mkuu wa Wilaya Iringa Richard Kasesela alikuwa Nyamihuhu kusikiliza kero za wananchi. Changamoto kubwa ilikuw ardhi ambapo kiji kimezungukwa na wawekezaji wenye ardhi kubwa ambao wamekuwa wanamiliki toka mwaka 1920 /1930.. Idadi ya wakazi imekuwa sasa maeneo yanazidi kuwa finyu. Pia wapo wananchi ambao wamekuwa wanauza ardhi. Pia wafugaji nao wana changamoto ya maeneo ya malisho. Suala la maji nalo lilibuka ambapo mradi wa kufuua maji unahitaji Tsh milioni 400. 
Mkuu wa wilaya aliahidi kufuatilia changamoto za maji jumatatu tarehe 18/04/16. suala la ardhi Mkuu wa wilaya aliagiza afisa ardhi apime upya maeneo pia uangaliwe uwezekano wa wewekazaji kupunguza maeneo na kuwagawia wananchi. Pia alishauri wafugaji wapunguze mifugo wanunue ardhi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo