UWT Mkoa wa Singida watangaza kumfanyia maandamano Rais Magufuli

JUMUIYA ya umoja wa wanawake (UWT) Tanzania mkoa wa Singida, unatarajia kufanya maandamano makubwa ya amani, kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli, kwa uwajibikaji wake ambao umefilisi kabisa hoja/ajenda zote za wapinzani.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida, Diana Chilolo, wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali ya siku tatu yanayohudhuriwa na Madiwani viti maalumu (CCM) kutoka halmashauri saba mkoani Singida.
Alisema wanawake wa mkoa huu wenye mapenzi mema na nchi yao, hawana budi kumpongeza na kumuunga mkono Rais Magufuli ambaye kwa muda mfupi, uchumi uliokuwa ukimilikiwa na watu wachache, umerejeshwa kwa wananchi.
UWT Singida“Nidhamu kwa watumishi wa umma, mashirika na Watanzania kwa ujumla, nayo chini rais Magufuli, imerudi. Sio hiyo tu,Rais wetu wa awamu ya tano kwa muda mfupi ameziba kabisa mianya yote ya rushwa na kubwa zaidi,uzalendo sasa umerudi upya”,alisema Chilolo na kushangiliwa kwa nguvu.
Diana Chilolo
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida, Diana Chilolo,akifungua wafunzo ya ujasiriamali ya siku tatu yaliyohudhuriwa na Madiwani wa Viti maalumu (CCM) mkoani hapa. Chilolo amewataka Madiwani hao kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye vikao mbalimbali kwa madai hayo, alisema watakuwa wamewajibika ipasavyo.
Alisema UWT itamshirikisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Martha Mlata na pia wamawake wote bila kujali itikadi zao za kisiasa,ili kwa umoja wao waweze  kumpongeza na kumtia moyo rais Magufuli,  aendelee na ujasiri wake wa kutumbua majipu bila kuchoka.
Kuhusu mafunzo ya ujasiriamali, Chilolo ametumia fursa hiyo kumpongeza mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida, Aysharose Matembe, kwa kuanza mapema kuwatumikia wanawake.
“Mbunge wetu Matembe, kwa ufadhili huu wa mafunzo ya ujasiriamali kwa waheshimiwa madiwani wote wa viti maalum mkoani kwetu, umeanza vema ….pamoja na kwamba yatawanufaisha madiwani, lakini nina uhakika wao nao watakuwa mabalozi wazuri wa kwenda kutoa elimu hii ya ujasiriamali kwa wanawake walioko kwenye maeneo yao”,alisema.
Aidha, mwenyekiti huyo alisema kuwa kitendo cha Matembe kumchagua yeye (Chilolo)  ambaye alichuana naye kwenye uchaguzi wa kugombea ubunge viti maalum mkoa hivi karibuni kufungua mafunzo hayo,kimeonyesha wazi kuwa ni mwanasiasa wa kweli.
Aysharose Matembe
Mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoa wa Singida, Aysharose Matembe,akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali  ya siku tatu yaliyohudhuriwa na madiwani viti maalum (CCM) mkoa wa Singida, yanayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi mjini hapa. Kwa Mujibu wa Matembe mafunzo hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika machi 8 mwaka huu. Walioketi katikati ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida, Diana Chiloli na wa kwanza kushoto ni Katibu UWT mkoa wa Singida,Anjela Mirembe.
Awali mbunge Matembe,alisema mafunzo hayo pamoja na ya ujasiriamali,pia yatakuwepo na ya utawala bora na ufugaji bora wa nyuki.
“Madhumuni makubwa ya mafunzo haya, ni kuwajengea uwezo na maarifa zaidi  madiwani wa viti maalum ili waweze kufanya ujasiriamali wenye tija na ambao utawakomboa kiuchumi.Nina imani kubwa kwamba diwani wa viti maalum akiwa na kipato cha kukidhi mahitaji,huyo atakuwa na uwezo mzuri wa kuwatumikia wanawake”,alisema.
Wakati huo huo, Mbunge Matembe alisema mafunzo hayo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inayotarajiwa kufanyika duniani kote Machi 8 mwaka huu.
Madiwani Viti Maalum Singida
Baadhi ya madiwani wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida,wakifuatilia mafunzo ya ujasiliamali ya ufugaji bora,ufugaji nyuki na ufugaji kuku.Mafunzo hayo yameratibiwa na kufadhiliwa na mbunge wa viti maalum mkoani hapa. (Picha na Nathaniel Limu).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo