Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imekamilisha zoezi la kuwahamisha kwenda vyuo vingine wanafunzi waliokuwa kampasi za Ruvuma na Arusha za Chuo Kikuu cha Matakatifu Joseph jijini Dar es Salaam baada ya kampasi hizo kubainika hazikidhi matakwa ya kutoa elimu ya juu.
Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo ya Vyuo Vikuu Profesa YUNUS MGAYA ambaye amesema miongoni mwa vyuo vikuu walivyohamishiwa wanafunzi hao ni Chuo cha Kilimo cha Sokoine SUA mjini Morogoro, Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM na Chuo Kikuu cha Ruaha