Waziri wa Kilimo Mifugoa na Uvuvi Mh Mwigulu Nchemba leo Jumamosi Marchi 05, 2016 amefanya ziara katika shamba la Mifugo la Mifugo la Makete mkoani Njombe kujionea utendaji kazi wa shamba hilo
Waziri Nchemba amekiri kufurahishwa na utendaji kazi wa shamba hilo na kuahidi kutendea kazi changamoto zote za shamba hilo na kusema katika kuelekea mwaka mpya wa fedha wa serikali yaani katika bajeti ijayo, anapita katika mashamba yote ya mifugo nchini kuona ni namna gani watafanya kazi kama serikali kuboresha sekta ya mifugo nchini
Hapa chini nimekuwekea picha zake
Waziri Mwigulu Nchemba (Mwenye skafu shingoni) akipita katika shamba la mifugo Kitulo kujionea utendaji kazi na ufugaji uliopo hapo
Waziri Mwigulu akitazama ng'ombe wa Kitulo
Ng'ombe wa Kitulo
Ndama wa shamba la Kitulo
Farasi wanaofugwa katika shamba hilo
Meneja wa shamba la Kitulo akisoma taarifa kwa Waziri Nchemba
Mbunge wa Makete Prof Norman Sigalla akizungumza katika ziara hiyo ya Waziri
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Daudi Yassin akizungumza kwenye ziara hiyo.
Waziri Mwigulu Nchemba akizungumza kwenye ziara yake katika shamba la mifugo la Kitulo
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa akizungumza kumshukuru waziri
Picha ya Pamoja (Picha zote na Edwin Moshi)