Mkuu wa wilaya ya Mvomero Betty Mkwasa amewasimamisha mawakala sita wa pembejeo za kilimo kwa kushindwa kuwajibika katika usambazaji wa mbegu katika kata za wilaya hiyo ambapo amemuagiza mratibu wa pembejeo wilaya kuvunja mkataba na mawakala hao na kuingia mkataba na wengine watakao weza kuwahudumia wakulima kwa wakati.