Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Sara Dumba amefariki dunia jana usiku katika hospitali ya Kibena Njombe
Sara Dumba wakati wa uhai wake
Akizungumzia kifo hicho Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt rehema Nchimbi amesema mkuu huyo wa wilaya jana alifika kazini kama kawaida na kufanya kazi zake lakini baadaye alijisikia vibaya na kupelekwa katika hospitali ya Kibena kwa matibabu zaidi na ndipo alipofikwa na umauti majira ya saa moja na Dakika kumi jioni
Mpaka sasa mkoa Unasubiri taatibu za mazishi pamoja na kuusafirisha mwili wa maehemu kwenda watakapoambiwa na familia
Dkt Nchimbi amesema mpaka sasa wakipata taarifa kutoka kwa familia ndipo watakapoandaa utaratibu wa kuaga mwili mkoani Njombe