Bodaboda Tandala Makete walia na Misumari ya Serikali

Madereva Wa pikipiki maarufu kama Bodaboda Pamoja na wamiliki wa Vyombo hivyo vya Usafiri wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa Kufuata taratibu zote za Umiliki wa Vyombo vyao Ikiwa ni Pamoja Na kusajili vyombo hivyo kabla Ya kuanza kufanya Biashara ya Kusafirisha Abiria Katika Maeneo mbalimbali wilayani hapa.

Hayo yamesemwa Mapema hii leo na Afisa Biashara Wilaya ya Makete Bw. Edonia Mahenge Ambae pia ni kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Wilaya ya Makete Wakati akizungumza na Vijana ambao ni waendesha Pikipiki Maarufu kama bodaboda pamoja na Wamiliki wa Vyombo hivyo waliofika Katika Ukumbi wa MTC Tandala kutoka katika Kata za Mang'oto. Ukwama. Na Tandala kwa lengo la Kutambuliwa na serikali kama Wafanyabiashara wa Bodaboda.


Vijana hao ambao ni waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda nao wakapata nafasi ya Kuuliza maswali yao kwa Viongozi hao hasa Afisabiashara bw, Edonia Mahenge Na Mkaguzi wa Magari Vehicle Inspector Frances Luwanga Ikiwa ni pamoja na Ufafanezi wa Usajiri wa Vyombo vyao,pamoja na leseni ya biashara.

Akijibu Maswali ya Vijana hao ambao ni wafanyabiashara wa Bodaboda Afisa biashara Bw, Mahenge amesema kuwa Kujisajiri kwa lengo la kufanya Biashara hiyo ni muhimu kwakuwa Bodaboda ni sawa na Biashara za aina nyingine.

Katika Kikao hicho wamehudhuria viongozi mbalimbali kutoka Wilayani Makete Akiwemo Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Makete Bw. Estomin Kyando, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Makete Mh, Egnatio Mtawa Pamoja na Maofisa wa Polisi wilaya ya Makete akiwemo Mkaguzi wa Magari wilayani Makete Vehicle Inspector Frances Luwanga Ambao kwapamoja Walipata nafasi ya Kuzungumza na Vijana hao wa Bodaboda.

Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya MAKETE bw, Estomin Kyando Amewataka vijana ambao ni wajasiliamali Wilayani Makete kujiunga katika vikundi mbalimbali ili kuweza kupata Mikopo kwa urahisi Hasa Pesa ambazo Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli aliahidi kutoa Kiasi cha Sh. Million 50 Kwa kila kijiji kote nchini.

Akitoa Ufafanuzi zaidi juu ya Matumizi ya Vyombo vya moto kwa Madereva wakiwa Barabarani Afande Luwanga amesema kuwa Nikosa kwa Dereva bodaboda Pamoja na Abiria wake kupanda pikipiki Bila kuvaa Kofia Ngumu maarufu kama Helmet na Kwayeyote atakayekiuka hatakama ni Abiria Atachukuliwa Hatua za Kisheria.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mh,  Egnatio Mtawa Amesema kuwa Vikao hivyo na Vijana amabo ni wajasiliamali vitakuwa vya mara kwa mara Huku akisema Suala la Askari Polisi Ambao hawana ubinadamu  kuwakamata Vijana hao wawapo barabarani Kisha Kuwanyanyasa Pasipo Maelewano Ni kosa Kisheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo