Mbunge wa Makete atoa Kauli ya Ujenzi wa Barabara ya Lami Makete-Njombe

Kutokana na wananchi wa Makete kuomba kwa muda mrefu kujengewa kwa kiwango cha lami Barabara ya Makete Njombe na ya Makete Mbeya, hatimaye mbunge wa jimbo la Makete amejitokeza hadharani na kuzungumzia suala hilo

Akizungumza na wandishi wa Eddy Blog mbunge wa jimbo la Makete Prof. Norman Sigalla King amesema kabla yeye hajaingia madarakani tayari serikali ilikwishafanya upembuzi yakinifu wa barabara ya Makete Njombe na kilichobaki sasa na ujenzi kuanza
Mbunge huyo amesema wananchi wategee sikio bunge la bajeti linalotarajiwa kuanza Aprili mwaka huu kwa kuwa wizara husika inataarifa njema kuhusu ujenzi wa barabara ya Makete  Njombe kwa kiwango cha lami

"Niseme tu hapa siwezi kutaja siku rasmi ya kuanza ujenzi wa hii barabara na badala yake niseme tu kwamba kila kitu kimekamilika kilichobaki ni serikali baada ya bajeti ya wizara ya ujenzi kupitishwa na bunge ambayo hiyo bajeti ina kipengele cha ujenzi wa barabara ya Makete Njombe kwa kiwango cha Lami, atatafutwa mkandarasi ambaye atapatikana kati ya siku 90 mpaka 120 akishapatikana ndipo ujenzi uanze, ninaimani baada ya bunge la Bajeti ujenzi huu wa barabara utaanza" amesema Prof. Sigalla
Kuhusu barabara ya Makete Mbeya kujengwa kwa kiwango cha lami amesema "Kwa kuwa hii imeahidiwa na Mheshimiwa rais Magufuli wakati akifanya kampeni, bado haijafanyiwa upembuzi yakinifu, tunategemea baada ya kumalizika kwa bunge la bajeti serikali itaanza kufanya upembuzi yakinifu wa barabara hii na majibu yake ndio yatatoa picha halisi ya gharama na ndipo serikali itoe fedha ianze kujengwa, haitaweza kujengwa bila kufanyiwa upembuzi yakinifu, tunawaomba wananchi muwe wavumilivu, serikali hii ya CCM ya awamu ya tano itafanya kama ilivyoahidi"

Hata hivyo ameongeza kuwa kwa sasa yeye ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge inayoshughulikia Miundombinu ambapo kwa sasa itazunguka katika maeneo mbalimbali ya nchi kufanya kazi yake ikiwemo kupitia wilaya ya Makete na maeneo mengine na moto wake wananchi watauona katika bunge lijalo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo