Mbunge wa Longido atajwa Mahakamani kuwa aliporomosha matusi

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya uchaguzi Jimbo la Longido mkoani hapa, Dk Stephen Kiruswa ameieleza Mahakama Kuu kuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi mwaka jana mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo hilo, Onesmo Ole Nangole alitumia lugha ya kibaguzi na propaganda dhidi yake.

Alidai ilimuathiri katika kipindi hicho cha kampeni na kusababisha kukosa ushindi.

Dk Kirushwa ambaye ni mlalamikaji katika kesi hiyo alidai hayo jana wakati akiongozwa na wakili wake, Dk Masumbuko Lamwai mbele ya Jaji Mfawidhi, Kanda ya Bukoba, Sivangilwa Mwangesi aliyepangiwa kusikiliza kesi ya Uchaguzi Jimbo la Longido Mkoani Arusha.

Alidai kauli za kibaguzi na propaganda zisizo za kweli alizokuwa akitumia mgombea wa Nangole zilimwathiri kwa asilimia 90 na ulikuwa ukiukwaji wa tataribu za uchaguzi.

Mgombea huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alidai kuwa Nangole alikuwa akifanya kampeni kwa kuwaeleza wananchi wa jimbo hilo ambao wengi wao ni wa jamii ya wafugaji kuwa yeye akichaguliwa atahamia nchini Marekani kwa kuwa si mmasai wa Longido.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo