Maiti yasahaulika Msikitini...Jeneza Labebwa Tupu bila Mwili

KATIKA hali isiyo ya kawaida, mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Manispaa ya Lindi, Nassoro Mkalawile, uliachwa Msikitini ambapo waombolezaji walibeba jeneza tupu na wakiwa njiani kwenda makaburini, wakabaini jeneza halikuwa na mwili.


Tukio hilo la kushangaza lilitokea wiki iliyopita kwenye Kata ya Raha Leo, saa 7:15 mchana, ambapo waombolezaji walibaini hali hiyo baada ya nguo iliyofunika jeneza kupeperushwa na upepo.


Hali hiyo ilimfanya mmoja wa waombolezaji kubaini mwili huo haukuwepo ndani ya jeneza.

"Samahani kidogo...naomba tushauriane, sijui macho yangu au vipi, nahisi humu ndani mwili wa marehemu haupo," alisema wakati akiwaeleza waombolezaji wengine.


Kutokana na hofu hiyo, waombolezaji walilazimika kuangalia ndani ya jeneza na kubaini mwili huo haupo ukiwa umesahaulika msikitini kwenye chumba kinachotumika kuoshea hivyo waliamua kurudi Msikitini ili kuuchukua.


Baadhi ya watu waliwatupia lawama  ndugu wa marehemu wakidai hawakuwa makini kuufuatilia mwili wa ndugu yao wakati ukioshwa.


Watani waliofahamika kwa majina la Myao Bakari na Daudi Mangupili, walisikika wakisema tukio lilifanywa makusudi ili kutoa fundisho kwa ndugu na jamaa wa marehemu wasirudie kudharau mila na desturi ikiwemo kutopeleka kwa watani barua ya kuwaarifu juu ya kifo hicho.


"Kwa kawaida mtu anapofariki, watani ndio hufanya shughuli zote zikiwemo za uoshaji mwili wake, watoto wa marehemu hawakufanya hivyo ndiyo maana leo tumewaonesha," alisema Mangupili.


Mwandishi wetu ambaye alihudhuria mazishi hayo yaliyofanyika katika makaburi yaliyopo eneo la Biti Sudi, katika kata hiyo, alizungumza na mjukuu wa marehemu, Nassoro Yusufu ambaye alisema kitendo hicho kimewapa fundisho.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo