Serikali wilayani Makete mkoani Njombe imetakiwa kushirikiana na jamii
kuhakikisha miradi mbalimbali inayofadhiliwa na wahisani na kutekelezwa katika
wilaya hii kuhakikisha inaendelea kufanya kazi hata kama wafadhili hao watajitoa
Hayo yamesema hapo jana wilayani Makete katika kikao cha asasi isiyo ya
kiserikali ya PADI kwa kushirikiana na wasaidizi wa kisheria wilaya ya makete
MADIPASE na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha wasaidizi hao wa kisheria
wanaendelea kufanya kazi zao wilayani Makete licha ya wafadhili wa mradi huo
kufikia kikomo chao Desemba Mwaka huu
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa
aliyeiwakilisha halmashauri yake katika kikao hicho amesema ni wakati wa jamii
kutambua kuwa miradi yote yenye ufadhili, wafadhili wana mwisho wake hivyo ni
wakati muafaka wa kuhakikisha wasaidizi hao wanaendelea kufanya kazi hata kama
wafadhili wanajitoa
Amesema
hawezi kutamka moja kwa moja katika kikao kicho kama halmashauri yake itatoa
kitu gani kwa wasaidizi hao wa kisheria ikiwemo suala la usafiri, na badala
yake wapeleke taarifa halmashauri na kupitia vikao halali majadiliano
yatafanyika na yaliyopo ndani ya uwezo wa halmashauri yatatatuliwa
Katibu wa MADIPASE akisoma taarifa
Akiikabidhi meza kuu
Bw Jackson kutoka PADI akiongea jambo
Wageni waalikwa wakisikiliza
Mh Mwandilava Diwani Kipagalo akichangia hoja
Mwenyekiti wa MADIPASE Mchungaji Sinene
Meza kuu ikisikiliza jambo
Wasaidizi wa kisheria Makete
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa