Askari wa Idara ya Uhamiaji mkoani Mara wamewakamata na kuwafikisha mahakamani raia saba wa Kenya kwa kosa la kuishi nchini na kufanya kazi ya Ualimu bila kibali.
Mwajiri wa walimu hao Charles Nyahula ambaye ni mmiliki wa Shule ya Vic Zone naye amepigwa faini ya Shilingi Milioni moja.
Hata hivyo Mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Mara Proches Kuoko amesema Idara hiyo inaendelea kuwasaka raia wa kigeni waliopo mkoani humo ambao wamekuwa wakifanya kazi bila vibali vya kuishi nchini.
Wimbi la Kuingizwa kwa wahamiaji haramu toka nchi mbali mbali limekuwa likiripotiwa Mara kwa Mara katika Maeneo mbali mbali Nchini huku Serikali ikiwachukulia Hatua Za Kisheria raia hao kutokana na Makosa waliyotenda.
Nao baadhi ya wahamiaji hao Haramu wamekiri kutenda kosa hilo na Kusema kuwa Wao hawakujua kufanya hivyo ni kosa.