Siku ya sheria: Mahakama ya Makete yaeleza kila kitu kuhusu sheria

Hali ya utendaji kazi wa mahakama katika wilaya ya Makete mkoani Njombe ni nzuri hususan katika kutekeleza agizo la serikali kuwa ipunguze kesi zilizokaa muda mrefu mahakamani na kwa kutenda haki

Hayo yamebainika leo katika kilele cha siku ya sheria ambacho kiwilaya kimeadhimishwa katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya Makete kikiwahusisha wadau mbalimbali ikiwemo mkuu wa wilaya ya Makete na wananchi wa wilaya hiyo

Akitoa hotuba katika maadhimisho hayo Hakimu mkazi mwandamizi wilaya ya Makete amesema ili haki itendeke kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake wakiwemo serikali, polisi, mawakili, mahakimu, washitaki na washtakiwa ambapo kwa pamoja wanahusika na kesi mbalimbali

Amesema inapotokea mmoja akashindwa kutimiza wajibu wake lawama zote hudondokea kwa mahakama kwa sababu wao wapo kwenye hatua ya mwisho ya kutoa maamuzi ama haki

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Makete Mh Daudi Yassin amesema anasikitishwa na kitendo cha mwitikio mdogo wa wananchi katika maadhimisho hayo huku akiiomba mahakama kutokatishwa tamaa na mwitikio huo na badala yake waendelee kuchapa kazi

Amesema amefurahishwa na kitendo cha mahakama kusema kuwa ipo huru na amesema waendelee na utendaji kazi wao kwa kutenda haki na wasiingiliwe na mtu yeyote katika ufanyaji kazi wao


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo