Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Makete hii leo limeazimia kuvunja rasmi mkataba wake na mkusanyaji mapato ya halmashauri hiyo
Hayo yametokea hii leo katika baraza la madiwani baada ya kuonekana anakiuka mkataba wake na halmashauri kuendelea kupata hasara katika ukusanyaji wa mapato
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mh Egnatio Mtawa ameiagiza bodi ya zabuni kukaa mara moja na kuona halmashauri itatakiwa kufanya nini ili mkataba huo uvunjwe mara moja bila kuathiri halmashauri
