Mtuhumiwa wa mauaji afia mahabusu

Mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dk. Sengondo Mvungi ameripotiwa kufariki akiwa gerezani, siku chache kabla ya kesi kusikilizwa.

Taarifa ya kifo cha mshtakiwa huyo aliyetajwa kwa jina la Chibago Chiuguta mwenye umri wa miaka 33, zilitolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kueleza kuwa mshitakiwa huyo alikutwa akiwa amekutwa na umauti.

Kufuatia taarifa hizo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Thomas Simba aliagiza upande wa Magereza kuhakikisha wanafuatilia cheti cha kifo cha mshitakiwa huyo.

Marehemu alikuwa kati ya washtakiwa 11 waliodaiwa kumuua Dk. Mvungi katika eneo la Msakuzi, Kiswegere katika wilaya ya Kinondoni. Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya kosa hilo Novemba 3 mwaka 2013.

Upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo