Mfanyabiashara auawa kinyama kisa laki saba tu

Wakazi wa Kijiji cha Kindi Tarafa ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani
Kilimanjaro, wakiwa kwenye mazishi ya marehemu Eugeni Mboro mfanyabiashara wa mahindi aliyeuawa kwa kukatwa na shoka nyuma ya shingo yake na kuporwa sh.700,000.
Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Anthony wa Padua, Kijiji cha Kindi Tarafa ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, Padri John Senya, 
 akiongoza ibada ya mazishi ya marehemu Eugeni Mboro mfanyabiashara wa 
 mahindi aliyeuwa kwa kukatwa na shoka nyuma ya shingo yake na kuporwa 
 
sh700,000.

Na Woinde Shizza,Moshi
WANANCHI wa Kijiji cha Kindi Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro wamesema ili kukomesha mauaji ikiwemo tukio la kukatwa na shoka nyuma 
 ya shingo kwa Eugeni Mboro kwa sababu ya sh. 700,000 wauaji hao 
 wachukuliwe hatua.

Mkazi wa kijiji hicho Richard Massawe alisema jana chanzo cha kifo hicho ni sh700,000 alizokuwa nazo Mboro baada ya kuuza mahindi yake
ndipo baadhi ya watu aliokuwa nao kupanga njama za kumuua na kuzichukua fedha hizo.

“Tunaomba serikali ichukue hatua kwani Mboro alikuwa ni mjasiriamali mdogo anayeibukia hapa Kindi na asiyekuwa na tatizo na mtu ila hao 
 kina Gasto na Kisimati walishikwa na tamaa ya kumuua ili wachukue 
 pesa,” alisema Massawe.

Mjomba wa marehemu Joseph Mwacha aliiomba serikali kuchukua hatua kwa wahusika wote wa mauaji hayo kwani ndugu yao hakudhulumu kitu cha mtu ila ni roho mbaya zilizosababisha kifo hicho na kumpora sh700,000 zake.

Hata hivyo, akiongoza ibada ya mazishi hayo, Paroko wa kanisa katoliki parokia ya Anthony wa Padua, Padri John Senya, aliwataka wakazi wa eneo hilo kupiga vita matukio ya uuaji kwa mtu asiye na hatia.

“Tunapaswa kubadiliwa jamani watu Kindi kwani itafikia siku mtu ukisema umetoka Kindi watu watakuangalia mara mbili mbili hivyo
unasema umetoka Kibosho badala ya kutaja eneo hili tulipozaliwa,” alisema Padri Senya.

Kwa upande wake, kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Ramadhan Mungi alisema mwili wa Mboro ulikutwa kwenye shamba la Michael Makabili huku akiwa na jeraha nyuma ya shingo lililotokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali.

Kamanda Mungi alisema pia marehemu aliibiwa fedha zake sh700,000 na wanawashikilia watuhumiwa wawili kwa uchunguzi akiwemo Gasto Costa (25) mkazi wa kijiji cha Kindi na mtu mwingine ambaye hakumtaja jina lake.


“Huyu mtuhumiwa Gasto tulifanya upekuzi kwenye nyumba yake na kukuta 
 kuna shuka lenye damu na nguo za marehemu Mboro ila huyu mtuhumiwa 
 
mwingine bado tunaendelea na uchunguzi juu yake,” alisem aKamanda 
 
Mungi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo