Waziri wa Elimu "apandishwa tena cheo" cha kitaaluma


WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imefafanua kuwa sifa ya kitaaluma ya waziri wa wizara hiyo ni Profesa Joyce Ndalichako; na siyo Dk Joyce Ndalichako.

Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam juzi na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha wizara hiyo, ilisema tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo wiki iliyopita, kwa bahati mbaya sifa ya kitaaluma ya waziri huyo, imeendelea kujulikana kama Dokta.

“Tunapenda kuufahamisha umma kwamba cheo cha kitaaluma cha Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Dokta Joyce Ndalichako kwa sasa ni Profesa Joyce Ndalichako”, ilisisitiza taarifa hiyo ya wizara

Taarifa hiyo ilisema wafanyakazi wa wizara hiyo, wanampongeza waziri kwa uteuzi huo na wanaahidi kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uadilifu katika kuendeleza sekta ya elimu na mafunzo nchini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo