Panga la Magufuli kuhamia kwenye vyombo vya habari...TCRA yatoa kauli

Katika kuendeleza kasi ya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imekusudia kuwafutia leseni wamiliki wa Radio na TV wanaokwepa kulipa ada zao sambamba na kwa makampuni ya simu yanayoshindwa kutoa huduma bora za mawasiliano kwa watanzania.

Hayo yameelezwa mjini Morogoro na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA, INJ.Dk Ally Yahaya Simba ambaye amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuhakikisha wanalipa ada zao za leseni na madeni mengine wanayodaiwa kabla ya Dec.30 mwaka huu, vinginevyo kuanzia Des 31 wataanza kufungiwa kwani kwa sasa wanadai takribani shilingi milioni 800 hao, huku akiwataka wamiliki wa mitandao ya simu za mkononi wanaotoa huduma zao chini ya kiwango na ubora unaotakiwa  kutoa huduma nzuri kwani kwenda kinyume watakabiliwa na adhabu kali sambamba na kuwafikisha mahakamani wote watakao toa huduma mbovu.
 
Nao wadau wa mawasiliano mkoani Morogoro wamewasilisha malalamiko mbalimbali kwa mamlaka hiyo hasa kwa upande wa mitandao ya simu za mkononi kukatà ovyo mawasiliano au kukata fedha tofauti na matumizi pamoja na kushindwa kushughulikiwa matatizo yao kwa muda muafaka huku wengine wakihoji matumizi ya watangazaji wasio na taaluma na weledi wakiwemo wanaoanzisha vipindi vilivyo kinyume na maadili ya mtanzania sambamba na usumbufu wa kutumia vingamuzi vingi tofauti katika matumizi ya TV.
 
Baada ya kupokea malalamiko hayo, mkurugenzi huyo ameahidi kufanyia kazi kwa kutoa adhabu kali kwa wale wote watakao bainika kwenda kinyume na maagizo na sheria za mamlaka ya mawasiliano Tanzania, sambamba na kuwa katika hatua za mwisho kununua mitambo ya kufuatilia matumizi ya simu ili serikali itoze gharama kwa makampuni ya simu kiusahihi na kukagua huduma za masafa kama zilivyoombwa na vyombo husika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo