Moto wateketeza uhai wa kijana huyu huko Arusha

Na Mahmoud Ahmad Arusha
MTU moja amefariki dunia , na vyumba vinne vya madarasa na ofisi mbili za walimu zikiteketea wa moto usiku wa kuamkia leo.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Edward  BaleLe, amesema matukio hayo yanatokana na vyanzo tofauti .

Amesema mtu mmoja ambae ni kijana amefariki kwa kuteketea kwa moto alipokuwa amelala kwenye nyumba ya mzazi  wake eneo la Njiro jijini Arusha.

Amesema kulingana na maelezo ya baba yake na marehemu, ambae ni mhadhiri mstaafu wa chuo ,mtoto wake alirejea majira ya saa tisa usiku  na kuingia ndani ya chumba chake na baada ya muda mfupi moto ulizuka na kuteketeza nyumba hiyo .

Amesema bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na chanzo cha tukio hilo.

Amesema moto huo unasadikiwa ulizuka majira ya saa kumi usiku wa kuamkia leo muda mfupi tu baada ya marehemu kuingia ndani ya nyumba hiyo na kulala na ndipo moto ulipozuka na kuteketeza nyumba hiyo.
Katika tukio lingine vyumba vinne vya madarasa vimeteketea kwa moto kwenye shule ya msingi ya Daraja mbili ya jijini Arusha.

Kamanda Balele, amesema  chanzo ni hitilafu ya umeme ambayo imesababisha pia  ofisi mbili za walimu kuteketea kwenye tukio hilo na hasara kamili bado haijajulikana.
Wakati huo huo kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Aruha, Philemon Mollel, ambae pia ni mgombea ubunge jimbo la Arusha, amefika kwenye shule hiyo na kuahidi tofali 2000 za Saruji.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo