Wagonjwa waliopata ajali wamelalamikia hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kukosa huduma ya muhimu ya X-ray na kulazimika kutafuta huduma hizo nje ya hospitali kwa gharama kubwa na wagonjwa wengine kukata tamaa kulazimika kurudi majumbani kwa kushindwa kumudu gharama.
Wagonjwa hao wamesema hali ya hospitali ya mkoa sio nzuri kwakuwa hospitali hiyo ndiyo pekee inayo tegemewa na wagonjwa wa kila sehemu hususani ikiwa nikiunganishi cha barabara kuu za mikoa mbalimbali ambapo wameiomba serikali kufanya jitihada za kununua mashine hizo ambazo ni muhimu sana kwa hospitali.
Akielezea changamoto hizo mganga mfawidhi wa hospital hiyo Dk Samsoni Tarimo amesema hospital ya mkoa wa Morogoro inakabiliwa na upungufu wa mashine ambapo wameomba serikali kuchukua hatua za kununua mashine zingine ilikunusuru hali hiyo ambayo imekuwa kero kwa wagonjwa.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu jimbo la Morogoro mjini Mh.Devota Minja akizungumza na uongozi wa hospitali hiyo baada ya kupewa tarifa ya uharibifu wa mashine hizo amesema ipo haja ya serikali kuangalia uwezekano wa kununua mashine nyingine kwani zilizopo zimetumika kwa muda mrefu na kuahidi kupeleka changamoto hiyo katika vikao vya bunge.
