Watu watu watano wamekufa ndani ya Saa 24, wawili wakiwa wameuawa na watu wasiojulikana usiki wa kuamkia leo hii katika manispaa ya Tabora, huku mmoja akiwa amefungwa mikono kwa nyuma na mwingine akitupwa katika eneo la reli itokayo mjini Tabora kuelekea mkoani Kigoma, na mmoja kujinyonga kutokana na kuibiwa debe moja la mahindi.
Akithibisha kutokea kwa matukio hayo mkoani Tabora hususani katika wilaya za Uyui,Urambo,Sikonge na Tabora manispaa, kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Hamisi Suleimani amesema kuwa, suala la mauaji mkoani Tabora linashika kasi na kuondoa amani na utulivu.
Aidha kamanda Hamisi akimtaja mama mmoja kwa jina la Hawa Haruna, aliyeibiwa nafaka zake na kusababisha kuwa na hasira na kuchukua jukumu la kuondoa uhai wake huko katika kata ya isira,kijiji cha mbola wilayani Uyui, amewataka watu wanaojihusisha na vitendo vya uporaji waache kabisa tabia hiyo kwani hawajui wenzao wanatafuta maisha kwa njia gani hali ambayo imeondoa uhai wa mtu.
Baadhi ya wananchi katika waliozungumzia mauaji ya kutisha katika manispaa ya tabora wamelaani vitendo hiyo kwani, ni kugubika shughuli za kimaendeleo kutokana na kuhofia kufanyiwa ukatili na watu wabaya.
Amewataja merehemu wengine,kwa majina ya Ramadhani Salumu aliyepigwa na radi akiwa mejiunganishia umeme wa Betri,radi ilipopiga eneo hilo akapitiwa, na mtoto wa miaka mitano Shabani Saidi,eneo la usoke,aligongwa na mwendesha pikipiki akafariki papo hapo.