Siku moja kabla ya kuapishwa rais mteule wa serikali ya awamu ya tano Dkt John Magufuli, aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha ukombozi na maendeleo-CHAUMA- Bw.Hashimu Rungwe amepanga kufungua kesi mahakama kuu ili iweze kutoa tafsiri ya inayotoa nguvu za kisheria kwa maamuzi ya tume ya taifa ya uchaguzi kutohojiwa au kupelekwa mahakamani.
Akizungumza na waandishi wa habari, aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha ukombozi na maendeleo-CHAUMA- Bw.Hashimu Rungwe amesema katiba ya nchi kifungu cha 107 kifungu kidogo cha kwanza kinasema mamlaka ya mwisho ya utoaji haki itakuwa mahakama, huku ibara ya 74 kifungu kidogo cha 2 kinasema hakuna mahakama yeyote itakuwa na haki ya kisheria kuchungua jambo lililo amriwa na tume ya uchaguzi hali inayotatanisha na kukiuka demokrasia.
Katika hatua nyingine waliokuwa wagombea ubunge katika jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Bwana Karama Masoud na chama cha mapinduzi Bwana Iddi Azzan pamoja na CHAUMA wamepanfa kufungua kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi kwa nyakati tofauti kwa madai ya kuwa uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa sheria ikiwemo kutishwa na kuondolewa kwa baadhi ya mawakala katika vituo wakati wa zoezi la kupiga kura pamoja na watu zaidi ya elfu 30 kunyimwa fursa ya kupia kura katika vituo 19 vya kupigia kura.