Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika tukio maalum na la kihistoria la kumwapisha rais mteule Dk John Pombe Magufuli na kumuaga rais anayemaliza muda wake Dk Jakaya Kikwete.
Sherehe hiyo itafanyika katika uwanja wa Uhuru ambapo amewataka wananchi hao kuanza kuingia uwanjani kuanzia saa 12 asubuhi na kwamba ulinzi umeimarishwa kila kona ya Dar es Salaam na kuongeza kuwa marais kutoka nchi nane wamethibitisha kuhudhuria na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali duniani.