Wakazi wa kigamboni jijini dsm , leo walipata wakati mgumu kwa upande wa usafiri , baada ya kivuko kimoja cha Mv-Magogoni kusitisha safari zake , hivyo kulazimika kutumia kivuko kimoja cha mv kigamboni.
Hali hiyo imetajwa kujitokeza majira ya asubuhi, muda ambao watu wengi wamekuwa wakivuka kutoka upande mmoja kuelekea mwingine , kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo kazi pamoja na biashara.
Blog hii imefika eneo la kivuko na kushuhudia umati wa watu wakitokea kigamboni ambao wamedai kuwa eneo hilo la Kigamboni limekuwa na hali tete kutokana na uwingi wa watu hatua ambayo imewalazimu watendaji katika kivuko hicho kuzuia magari kuvuka kwa kutumia kivuko hicho ili kupunguza uwingi wa abairia.
Wakizungumzia kadhia hiyo baadhi ya abiria wamesema hali hiyo imewafanya baadhi ya watu kushindwa kabisa kuvuka kutoka kigamboni kuja posta hususan wanafunzi.
Hata hivyo mamlaka husika hazikupatiikana kuzungumzia tatizo hilo la kivuko cha MV Magogoni