Hali ya mtafaruku iliikumba shule ya msingi ya Balita iliyopo Wilaya ya Mayuge nchini Uganda baada ya wazazi wenye hasira kuvamia shule hiyo na kuanza kuwachapa bakora walimu.
Wazazi hao walivamia shule hiyo Ijumaa jioni baada ya kupata taarifa kuwa mwalimu Robert Gidudu alimchapa fimbo hadi kufa mwanafunzi Sharifa Nabagala, wa darasa la sita.
Walimu hao walinusuriwa na polisi kutoka kituo cha polisi Kati cha Mayuge, ambao walipewa taarifa ya kichapo hicho waliokuwa wakipatiwa walimu na wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo.
Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Moses Mwase, alisema wazazi hao walikuwa na mawe pamoja na fimbo na walianza kuwapiga walimu kwa kuwatuhuma za kumuua mwanafunzi huyo.
