Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya tukio hilo kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Fednandi Mtui alisema kuwa mwanajeshi huyo feki alikamatwa jana eneo la kazuramimba katika Wilaya ya uvinza.
Mtui alisema kuwa mwanajeshi huyo alitambulika kwa jina la James Charles miaka 27 mkazi wa kijiji cha Nyamori alikamatwa baada ya kuwepo kwa taarifa kutoka kwa raia wema juu ya utapeli aliokuwa akiwafanyia na kuwekewa mtego na kukamatwa.
Kamanda alisema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa na kuulizwa alipozitoa sare hizo alisema kuwa yeye ni dobi wa kufua nguo,hivyo huvaa sare hizo pale anapoletewa na wateja kwaajili ya kuzifua.
Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika,pia jeshi la polisi limetia wito kwa wananchi wote ambao wameshatapeliwa na mtuhumiwa huyo kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi kilichopo jirani yao.