Mkuu wa wilaya atangaza atakavyo "deal" na hospitali na polisi

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda leo amenisogezea stori nyingine na kikubwa anachokigusia ni kuhusu kuzindua huduma kwa wananchi ambazo zitawasaidia kwenye  maeneo mbalimbali, najua ni wengi wanakutana na matatizo kwenye ofisi za umma ikiwemo Polisi, Hospitali na kwingineko…


Majibu ya nini kitafanyika yako hapa >>> “Kutokana na kero nyingi zinazoendelea na kusababisha watu kukosa huduma, watu wanapiga simu polisi wakiomba msaada kutokana na kuvamiwa, wanaambiwa waweke mafuta kitu ambacho si kazi yake, mtu anakwenda hospitali anakaa siku mbili au tatu hamuoni nesi, ardhi mtu anafatilia kibali cha kujenga zaidi ya miaka mitatu hapati, sisi hatuoni kama kuna sababu ya haya kuendelea kufanyika
Sentensi za Paul Makonda zinaendelea hivi >>> Tunaanzisha mfumo utakaowasaidia wananchi kupata misaada kutoka Serikalini , mfano umekwenda hospitali hupati msaada, unachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwa kuandika ujumbe mfupi kwenda namba 15404 na baadaye utapata ujumbe kutoka kwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na utafanyiwa kazi na wahusika kushtakiwa“.
DC Paul Makonda amesema kingine ni kwamba utaratibu unaoanzishwa sasahivi Wakurugenzi wa kata watapewa taarifa kuhusu malalamiko ya kila eneo husika na kuwaonyesha malalamiko yanayotolewa na wananchi wa maeneo yao.
Ujumbe wote kutoka kwa DC Paul Makonda utausikia ukibpnyeza play hapa…


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo