KIAPO: Kassim Majaliwa Aapishwa Rasmi Ikulu Ndogo Dodoma Kuwa Waziri Mkuu



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli,asubuhi hii amemuapisha Mbunge wa Ruangwa, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mjini Dodoma.

Hafla ya Kumuapisha Mh. Majaliwa imefanyika kwenye Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo, Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. samia Hassan Suluhu, Rais wa Zanziba, Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais Msitaafu, Dk. Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Wabunge, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, Wabunge na wageni wengine.

Tazama  Video  hii  Kushuhudia tukio hili 



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo