Hot news: CHADEMA washinda kesi ya Mawazo

Taarifa kutoka Mahakama kuu kanda ya Mwanza zinaarifu kuwa Familia ya Alphonce Mawazo na Chadema wameshinda kesi dhidi ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mwenyekiti huyo  wa Chadema Geita asiagwe  jijini Mwanza baada ya kuuawa kinyama kwa kukatwa mapanga 

Amri ya Jeshi la polisi kuwa Mawazo asiagwe Mwanza kwa kuwa kuna hofu ya kipindupindu imetupiliwa mbali na Mahakama hiyo. 

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Lameck Mlacha imetoa ruhusa mwili wa Alphonce Mawazo kuagwa jijini Mwanza na imeagiza Jeshi la Polisi kutoa Ulinzi siku hiyo lakini Ulinzi huo usivuke mipaka.

Sehemu ya hukumu ya kesi hiyo inasema "Kazi ya Polisi ni kulinda raia na si kuzuia mazishi.."IMG_0006


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo