Aliyekuwa mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Maendeleo ya Umma (CHAUMA), Hashim Rungwe ataka kwenda mahakamani kwa kile kinachosadikiwa kupinga matokeo ya Urais. Mgombea huyo mwenye taaluma ya Uwakili pia alisema kuwa baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Urais alipokea salamu nyingi sana za pole tofauti na idadi ya kura alizopata na kutangazwa hivyo kudai ni dhahiri kuwa aliibiwa kura, kitendo kilichofanya asiweze kushinda kiti cha Urauis alichokuwa akikigombania.
Wakati huohuo, Hashimu Rungwe alisema anadhamiria pia kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba Mahakama hiyo itoe/impatie fasiri ya kwanini Tume ya Taifa ya Uchaguzi haiwezi hojiwa na kupingwa mahakamani pindi itangazapo matokeo ya Urais.