Jeshi la polisi mkoani Pwani linamshikilia Mganga
Mfawidhi Ramadhan Mtambo wa zahanati ya kijiji cha Mkongo
Kaskazini kilichopo Wilayani hapa kwa tuhuma za kupatikana Kaskazini kilichopo Wilayani hapa kwa tuhuma za kupatikana
na dawa za binadamu bila kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, kamanda Jafari Mohamed
alisema Mganga huyo alikamatwa na mwenyekiti wa kijiji hicho
Mussa Mohammed Sungu majira ya saa 9:31 Alasiri katika kituo
cha Afya Kibiti siku ya jumatatu.
Alisema Mganga huyo alikamatwa na boksi kumi na tatu za
dawa za kutibu Malaria aina ya Artemether and Lumefantrine
maarufu kwa jina la Mseto kukiwa na dozi 390 za kutibu
ugonjwa huo.
Kamanda Jafari alisema dawa hizo zilikuwa na thamani ya shilingi 975,000 za kitanzania na
zilikuwa zimepelekwa katika zahanati ya kijiji hicho siku chache kabla ya tukio.
Alisema,Mganga huyo alipohojiwa ni wapi alipokuwa akizipeleka dawa hizo,Dr Ramadhani
Mtambo alijibu alikuwa akizipeleka katika kituo cha Afya Kibiti kwa ajili ya kubadilishana dawa
hizo na dawa za kushusha msukumo wa damu (B P)
Alisema baada ya kutokea mvutano kati ya Mganga huyo na Mwenyekiti wa kijiji hicho,
kulipelekea Mganga huyo kumshambulia Mwenyekiti huyo kwa bakora baada ya kubaini mpango
wake umeharibika.
Kamanda Jafari alifafanua kuwa kufuatia mvutano huo askari polisi waliitwa ambapo walifika na
kumkamata Mganga huyo hadi Kituo cha Polisi Kibiti ambapo baada ya kuupekuwa mfuko
aliokuwa nao walikuta una dawa hizo za kutibu malaria box kumi na tatu.
Kamanda Jafari alieza kuwa walilazimika kumuita Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Kibiti Dr
Jones Chagi kwa ajili ya kuja kutoa maelezo ya madai yaliyotolewa na Mganga huyo,lakini alikana
hakuwa na makubaliano yoyote na Mganga ya kubadilishana dawa.
Akizungumzia mkasa huo,Mwenyekiti huyo Mussa Mohammed Sungu alisema alimshitukia
mganga huyo huenda amebeba dawa hizo hivyo kulazimika kumfuatilia kwa pikipiki hadi
alipomkuta katika eneo la Corecu Kibiti.
Alisema baada ya kumuona alisimamisha pikipiki yake kisha kuanza kumhoji na baadaye kukata
fimbo na kumshambulia maeneo mbalimbali mwilini mwake,kabla ya kutaka kukimbia na
kuutelekeza mfuko huo ambapo watu walijitokeza na kumsaidia kumkamata mganga huyo.
