CUF watoa ufafanuzi kuhusu wabunge wake kuzomea bungeni

Chama cha wananchi CUF kimetoa ufafanuzi kuwa wabunge wake walilazimika kutoka nje bungeni na kushiriki zomea zomea muda mfupi kabla Rais John Magufuli kulihutubia bunge siku ya ijumaa na kusema hatua hiyo inafuatia wao kutaka kupaza sauti kwa umma kwamba hawamtambui Dk Ali Mohamed Shein kama rais wa Zanzibar.

Akitoa taarifa ya pamoja ya wabunge wote wa CUF katibu wa wabunge wa CUF bungeni Mh Hamid Bobali amesema nia ya wabunge wa UKAWA haikuwa kufanya vurugu ndani ya bunge bali ni kupaza sauti kwa serikali kuharakisha kutanzua mkwamo wa kisiasa visiwani zanzibar.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo