Jeshi la polisi mkoani Tanga
linamshikilia aliyekuwa askari wake Bw Antoni Temu miaka 46 kwa tuhuma za
kushawishi na kuchukua rushwa kutoka kwa dereva wa gari katika kijiji cha
Kilumbo wilayani Handeni mkoani Tanga
Kwa mujibu wa kamanda wa
polisi mkoani Tanga Zuberi Mwombeji askari huyo anachukuliwa hatua za kisheria
na tayari ameshafukuzwa kazi na kwa sasa yupo mahabusu akisubiri kupelekwa
mahakamani
Tukio hilo limetokea jana
majira ya saa saba mchana kwenye eneo la barabara ya Segera - Chalinze, na leo
asubuhi jeshi hilo limetangaza kuwa limemfukuza kazi na hatua za kisheria za
kumfikisha mahakamani zinafanyika
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza kamanda wa polisi mkoani Tanga, Zuberi Mwombeji akizungumza kuhusiana na askari huyo kukamata na kukabidhiwa kwaTAKUKURU.
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza kamanda wa polisi mkoani Tanga, Zuberi Mwombeji akizungumza kuhusiana na askari huyo kukamata na kukabidhiwa kwaTAKUKURU.