Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Ubungo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Saed Kubenea ameibuka mshindi katika jimbo hilo kwa kuwabwaga wagombea wenzake akiwemo mshindani wake wa karibu Didas Masaburi wa CCM
Matokeo hayo ambayo yametangazwa rasmi mchana huu, yamesema kuwa kubenea amepata ushindi wa kura 87, 606 ambazo hazijafikiwa na mgombea mwingine yeyote wa jimbo hilo