Rais Kikwete azindua shule ya WAMA huko Lindi



 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiondoa kitambaa kwa kushirikiana na Bwana Ibrahim Sharaf aliyefadhili ujenzi wa Shule ya Wasichana ya WAMA Sharaf ikiwa ni ishara ya kuizindua rasmi. Baadaye Rais Dkt. Kikwete akishirikiana na viongozi wengine walisaidia ujenzi wa shule hiyo kukata utepe ikiwa ni mwendelezo wa sherehe za ufunguzi rasmi wa shule hiyo huko Lindi tarehe 11.10.2015.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwa wamekaa kwenye mojawapo ya madawati ya wanafunzi na Bwana Ibrahim Sharaf, Mwenyekiti wa Sharaf Group of Companies (wa kwanza kushoto) na ndugu yake Bwana Sharafuddin Sharaf ( wa kwanza kulia) wakati wanatembelea sehemu mbalimbali za shule.
Rais DKT. Jakaya Kikwete akifuatana na Bwana Sharafuddin Sharaf na wageni wengine wakitembelea shule.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na wageni waalikwa wakiangalia wanafunzi wakifanya majaribio mbalimbali ya masomo ya sayansi kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Sharaf huko Lindi baada ya kufunguliwa rasmi tarehe 11.10.2015.
 Rais DKT. Jakaya Kikwete na Mama Salma wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi walioshiriki kufanya majaribio ya masomo ya sayansi.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Daud Nassib jinsi wanafunzi watakavyotumia  kompyuta zilizofungwa kwenye shule hii ili kufanikisha masomo yao.


Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma wakiwatembeza wageni waalikwa sehemu mbalimbali za shule hiyo.

Baadhi ya waalikwa kwenye sherehe ya ufunguzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana WAMA Sharaf huko Lindi wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa sherehe za ufunguzi wa shule hiyo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kwa viongozi na wageni waalikwa wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa Shule ya WAMA Sharaf huko Lindi tarehe 11.10.2015.
Mwakilishi wa Sharaf Group of Companies Bwana Sharafuddin Sharaf akitoa hotuba yake kwa niaba ya kampuni wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa shule hiyo iliyojengwa na kampunio yake huko Lindi.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake ya uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari ya WAMA Sharaf iliyojengwa na Kampuni Sharaf kutoka Dubai huko Lindi tarehe 11.10.2015.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akitoa tunzo maalum kwa Kampuni ya Sharaf Group ya Dubai kwa msaada wao wa kujenga shule hiyo huko Lindi.
PICHA NA JOHN LUKUWI  


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo