Mgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Ndugu Estomih Malla amefariki dunia usiku wa leo saa saba katika hospitali ya KCMC Moshi.
Ndugu Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa sababu ya kupata tatizo la shinikizo la juu la damu.
Hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni,ambapo alilalamika kusikia kizunguzungu na baadae kukimbizwa hospital ya St Thomas ambapo madaktari wa pale walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu.
Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho. Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya uongozi wa chama hicho kufanya mawasiliano na viongozi waliopo mkoani Arusha.